Katika kutambua kazi kubwa inayofanywa na wanawake viongozi ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani wanawake wa Manispaa hii wamemvisha taji la malkia wa nguvu Mstahiki Meya wa kwanza mwanamke aliyewahi kuongoza Manispaa hii Bi. Shadida Ndile.
Shadida ametunukiwa taji hilo Machi 7,2021 kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa.
Pamoja na taji hilo Wanawake hao walimuandalia keki Pamoja na zawadi mbalimbali ili kutambua mchango wake kwa wanawake.
Akizungumza mara baada ya kupokea zawadi hizo Bi. Shadida amewashukuru wanawake wote walioandaa sherehe hizo na kumuandalia zawadi.
Amesema kuwa jambo hilo kwake limekuwa ni deni ambalo anatakiwa kulilipa kwa kufanya kazi kwa bidii katika kuiletea Maendeleo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Shadida Ndile amestahili kuwa malkia wa nguvu kw akuwa ni Meya pekee mwanamke anayeongoza halmashauri hapa nchini, ni mstahiki Meya wa kwanza mwanamke kuwahi kuongoza Manispaa ya Mtwara-Mikindani lakini pia ni Diwani pekee mwanamke anayeongoza Kata Kati ya Madiwani kumi na nane.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.