Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Shadida Ndile ameonesha kuchukizwa na tabia ya wananchi kutohudhuria mikutano ya hadhara na kuwataka wananchi hasa vijana kujitokeza kwa wingi katika mikutano inayoitishwa kwenye Kata na Mitaa kwani mikutano hiyo ni fursa mojawapo ya kuwasilisha kero zao kwa watendaji wa Serikali.
“Sijaridhishwa na mahudhurio yenu, mahudhurio ni madogo sana hasa vijana tusitumie vijiwe kulaumu Serikali tulete kero zetu katika mikutano hii” Amesema Ndile.
Mhe. Ndile ametoa rai hiyo Oktoba 7, 2021 katika Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga na wananchi wa Kata ya Mtonya.
Amesema kuwa Serikali imeweka utaratibu wa mikutano hiyo ili kuwaleta wananchi na watendaji wa Serikali pamoja katika kupeana taarifa mbalimbali za maendeleo katika Kata na Manispaa Yetu.
Aidha amewataka wananchi wa Kata ya Mtonya kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa ili kupata ulinzi wa matibabu .
“Tunaishukuru Serikali kwa kutuletea Mfuko wa Bima ya afya iliyoboreshwa Bima nitoe rai kwa wananchi tujiunge na Mfuko wa Bima iliyoboreshwa, kuna faida kubwa sana utaipata” Amesema Ndile
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.