Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara -Mikindani Mhe. Shadida Ndile amewataka washiriki wa kikao cha Uhamasishaji wa Mpango Harakishi wa chanjo ya COVID -19 kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO -19 ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo katika Manispaa yetu.
“Serikali imewaamini nendeni mkashirikiane katika kuhakikisha elimu hii inaifikia jamii husika ili tuweze kudhibiti ugonjwa huu” Amesema Ndile
Mhe. Ndile ametoa rai hiyo Oktoba 2, 2021 katika kikao cha Uhamasishaji wa Mpango Harakishi wa chanjo ya COVID -19 kilichoshirikisha Madiwani, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Watendaji Kata na wa Mitaa , Maafisa maendeleo ya Jamii pamoja na Maafisa Afya Kata wa Manispaa ya Mtwara - Mikindani.
Amesema kuwa elimu hiyo ikitolewa kwa umakini na usahihi itaondoa imani potofu ambazo zinaendelea kusambazwa katika jamii juu ya madhara yatokanayo na chanjo ya UVIKO -19.
Sambamaba na hili amewataka washiriki hao wasikate tamaa watakapokutana na changamoto katika jamii wakati wa zoezi la uhamasishaji kwani kwenye mafanikio daima kuna changamoto
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hassani Mtenga amewataka washiriki hao kuendeleza jitihada dhidi ya mapamabano ya ugonjwa wa UVIKO -19 ili jamii yetu ibaki salama.
Naye Mratibu wa Kuthibiti Ukimwi Wilaya Nae Dkt. Lusungu Mselela amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kutoa elimu ya UVIKO -19 kwa washiriki hao ambayo ikitumiwa kwa usahihi itazuia maambukizi mapya ya ugonjwa wa UVIKO -19.
Bi. Zuhura Musa ambae ni mshiriki wa kikao hicho, ameishukuru Serikali kwa kuratibu mafunzo hayo kwani kwa kupitia elimu hiyo iliyotolewa ameongeza maarifa zaidi juu ya UVIKO -19.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.