Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe.Shadida Ndile leo tarehe 29 Oktoba 2024, ameiongoza Kamati ya Fedha na Uongozi kutembelea na kukagua Maendeleo ya miradi mbalimbali inayoendelea ndani ya Manispaa hiyo.
Katika ziara hiyo kamati imetembelea na kukagua Maendeleo ya mradi wa ukamilishaji wa Ujenzi wa bweni la Shule ya Sekondari Naliendele, pamoja na Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu (2 in 1) Shule ya Sekondari Mkanaredi inayotekelezwa na Serikali Kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
Miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa majengo matano ya hospitali ya Wilaya Mjimwema unaohusisha Jengo la mama na mtoto (Matenity Ward), Jengo la dawa (Phamarcy), Jengo la Mionzi (x-ray), Jengo la umeme (Power house) pamoja na Ofisi ya Ulinzi (Security house).
Aidha kamati pia imetembelea Ujenzi wa Shule ya Sekondari Tandika pamoja na Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi wa Manispaa unaoendelea katika mtaa wa Shangani West.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.