Kuelekea kwenye Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia itakayozinduliwa Novemba 25 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Col. Abbass Ahmed Abbas kwa kuongea na vyombo vya Habari Mkoani hapa, Timu ya ulinzi na Usalama wa mtoto Manispaa ya Mtwara-Mikindani imetembelea kwenye Kata mbalimbali na kuzungumza na watendaji wa Kata husika lengo ikiwa ni kuangalia namna Ofisi hizo zinavyotekeleza masuala ya ulinzi na Usalama wa mtoto kwa kutatua masuala ya ukatili kwa Watoto na wanawake.
Katika ziara hiyo timu imebaini uwepo wa uendelevu wa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ambapo wanajamii ,wazazi wanawafanyia Watoto na Watoto kwa watoto wenyewe wanafanyiana masuala ya ukatili.
Afisa Ustawi wa Jamii Bwana Godlove Miho amesema kuwa Ofisi ya Mkurugenzi kupitia timu hiyo inaendelea na utoaji wa elimu juu ya ukatili dhidi ya wanawake na Watoto na kwa kushirikiana na dawati la jinsia itaendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wote watakaobainika kukiuka haki za watoto na wanawake.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.