Mbunge wa Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga, leo (Novemba 25,2024) amekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh Milioni 40.7 katika kituo cha afya cha Likombe kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ili kuboresha huduma za afya kituoni hapo.
Akizungumza na wananchi na watumishi wa Afya katika kituo hicho, Mhe. Mtenga aliwataka watumishi hao kuvitunza na kuvitumia kwa umakini mkubwa ili vitumike kwa mda mrefu, wakati Serikali ikiendelea kutatua changamoto zingine zilizopo kituoni hapo.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na vifaa vya kujifungulia wajawazito (Delivery kit) - 10, Makabati katika vitanda vya wagonjwa (Bedside Locker) -15, Mashuka ya wagonjwa - 60, Nguzo za kusimamishia Dawa (Drip stands) -15, Meza za Uchunguzi (Examination Table) - 7, Vitanda vya wagonjwa - 15, Magodoro - 15 na Meza za juu ya vitanda vya wagonjwa (Over Bedtable) - 8.
Awali akisoma taarifa fupi kwa Mgeni Rasmi, Dkt. Kalume Nyambi amesema kuwa uwepo wa vifaa tiba vyenye uhakika vitasadia kiasi kikubwa mkakati wa taifa kupunguza idadi ya vifo kwa wajawazito na Watoto wachanga.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Likombe Mhe. Saidi Seif amemshukuru Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kuwaletea vifaa tiba mbalimbali huku akimuomba Mbunge kupitia serikali kuboresha miundombinu ya majengo ya kituo hicho ikiwemo jengo la wagonjwa wa nje (OPD), vyumba vya kulaza wagonjwa, Kichomea taka pamoja na ujenzi wa uzio ili kuhakikisha usalama wa watumishi, wagonjwa na mali za kituo hicho.
Naye Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo, Dkt. Elizabeth Oming'o amemshukuru Mhe. Mtenga kwa kuleta vifaa hivyo kwani vitasaidia kuboresha huduma kwa wananchi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.