Mbunge wa Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga, amechangia matofali 1000 pamoja na mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya kuongeza nguvu ujenzi wa uzio katika shule ya sekondari chuno, kata ya Chuno, ujenzi ulianza kutokana na juhudi za wananchi wa kata hiyo.
Sambamba na hilo Mhe. Mtenga pia amechangia jumla ya mabati 50 za geji 28 ili kukarabati paa za baadhi ya madarasa yaliykuwa yakivuja na kuleta kadhia kwa wanafunzi kipindi cha mvua.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mbunge, Katibu wa Mbunge, Hassan Salum “hans” alisema lengo kuu la msaada huo ni kuboresha kiwango cha ufaulu kwa kuimarisha ulinzi wa wanafunzi shuleni hapo.
Alisema Mbunge anapenda sana maendeleo ya wananchi wa kata zote ndio sababu hajasita kuwaunga mkono wakazi wa Chuno kutekeleza Mradi huo ambao pia unakwenda kulinda Samani za shule hiyo.
Mbali na msaada huo alisema Mtenga pia alishajitolea Mashine moja ya photocopy katika shule hiyo na kuahidi kuendelea kuboresha zaidi.
Naye Diwani wa kata hiyo Mhe. Fanikiwa Chijinga, alimshukuru Mbunge kwa msaada huo na kutoa rai kwa wadau wengine zaidi kuendelea kuchangia juhudi hizo za wananchi kwani hadi kukamilika uzio unahitaji takribani matofali 14000 na mifuko ya saruji 686.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.