“MTU ANAPOKUJA KWA LENGO LA KUKOSOA MPOKEE NA TUKUBALI KUKOSOLEWA’MONGOGWELA
Maafisa malalamiko wametakiwa kuwapokea wananchi wanaofika ofisini kwa lengo la kukosoa serikali na kukubali kukosolewa kwa kuwa ni njia moja wapo ya kuimarisha mahusiano na utawala bora.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Renatus Mongowela kwenye ufunguzi wa mafunzo ya ushughulikiaji wa malalamiko yaliyofanyika katika Ukumbi wa hoteli ya Tiffany Septemba 25, 2017.
Amesema kuwa utawala makini ni ule unaohakikisha kuwa kunakuwa na mawasiliano kati ya Wananchi na Serikali yao,Wananchi wanayohaki ya kuchangia mawazo na michango yao kwa serikali hivyo ni lazima kuhakikisha kuwa mawazo ya Wananchi hao yanajadiliwa na kutatuliwa.
Amesisitiza Maafisa malalamiko kuwajengea mfumo wananchi waweze kutoa mawazo yao bila woga, kwani Mwananchi anaetoa maoni na mawazo yeye ni mdau mkubwa wa maendeleo na amekubali
Aidha amewataka Maafisa hao kuhakikisha Malalamiko yote yanayoshughulikiwa ni lazima yarekodiwe na kutunzwa vizuri kwenye rejista kwani yawezekana afisa anayeshughulika malalamiko hayo kuhama hivyo kusaidia atakayeshika nafasi yake kuwa na mwanzo nzuri pindi anapofika mteja ambaye tayari alishashughuliwa awali kwa lalamiko lilelile.
Hata hivyo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa makini na malalamiko wanayoyashughulikia na kama kuna ugumu kwenye utatuzi wa lalamiko hilo wasisite swala hilo kulipeleka mbele zaidi.
“Ninawaasa muda wowote mnapoona lalamiko lililotolewa huwezi kulitatua usisite kulipeleka mbele na likipatikana ufumbuzi mrejesho utolewe kwa muhusika”alisema Mongogwela.
Mongowela amatoa rai kwa washiriki wa mafunzo hayo kuwa elimu waliyoipata kwenye mafunzo hayo isiishie hapo badala yake isambazwe kwa kwa wnaopata huduma ambao ni Wnanachi.
Awali akitoa taarifa fupi ya Mradi uliofadhili mafunzo hayo mwakilishi kutoka katika shirika la ps3 ndugu Peter Kilima alisema kuwa Mradi wa uimarishaji Mifumo kwa sekta za umma umefanya shughuli nyingi mpaka sasa ikiwemo utoaji wa mafunzo kwa Madiwani, Imeanzisha Tovuti kwa halmashauri 123 za Tanznaia bara ,umetoa mafunzo ya Plan Rep ,umetoa mafunzo kwa watoa huduma vituoni namna ya kupanga matumizi kwenye mfumo wa kuangalia fedha vituoni(sektaya Afya na Elimu)
Nae Lulu Ngachinja Diwani viti maalumu Manispaa Mtwara-Mikindani amabe pia ni mshiriki wa mafunzo hayo ameahidi kiyafanyia kazi mafunzo hayo na kuyatekeleza kwa vitendo yale yote yatakayofundishwa.Aidha aliwashukuru shirika la usimamizi wa mifumo katika sekta za umaa kwa kuwapa mafunzo hayo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.