Juni 4,2022 Manispaa ya Mtwara-Mikindani imepokea awamu ya kwanza ya pembejeo za ruzuku ya zao la korosho 9118 kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa uzalishaji wa zao hilo kwa mwaka 2021/2022.
Baada ya kupokea pembejeo hizo Manispaa imekabidhi kwa kamati za ugawaji za kwenye Kata ili waweze kuzigawa kwa wakulima.
Pembejeo zilizopokelewa ni Pamoja na sulphur ya unga mifuko 362, viuatilifu vya sumu (Subachlo 234 L), Viuatilifu vya sumu(Mocron) 74L, Viuatilifu vya Kudhibiti UbwiliUnga (dual Purpose Indazoel 2984L).
Pembejeo zingine ni Pamoja na Viuatilifu vya kudhibiti UbwiriUnga (Single Purpose) Movil851L, Subatex2 040, Balaki 1573L.
Hii ni Habari njema kwa wakulima kwani pembejeo hizi zinatolewa bure na Serikali na kupelekwa kwa wakulima isipokuwa mabomba ya kupulizia viuatilifu hivyo ambapo mkulima atachangia nusu ya gharama ya bei halisi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.