Mbunge wa jimbo la Mtwara Mjini Mhe.Hassan Mtenga Septemba 27, 2021 amekabidhi fulana 22 kwa kikundi cha Wanawake Mtwara Kuchele kinachofanya usafi wa mazingira Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Akikabidhi fulana hizo kwa niaba yake , Ndg. Hassan Namkami ambae ni Katibu wa Mbunge wa jimbo la Mtwara Mjini amesema kuwa Mhe. Mtenga anatambua jitihada zinazofanywa na kikundi hicho katika kuhakikisha Manispaa ya Mtwara –Mikindani inakuwa na mazingira safi.
“Inawezekana kazi mnayofanya ni kubwa kuliko mnachokipata, Mhe. Mtenga anathamini jitihada zenu na yupo tayari kuwaunga mkono” Amesema Namkani
Sambamba na tisheti hizo Mhe. Mtenga ameahidi kuwasaidia vifaa vya usafi pamoja na bima ya afya kwa kila mwanachama wa kikundi hicho.
“Mhe. Mtenga amenituma niwaambie atawasaidia vifaa vya kufanyia usafi pamoja na bima ya afya itakayomwezesha kila mmoja kupata huduma ya afya kwa gharama nafuu” Amesema Namkani
Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha Mtwara Kuchele Bi. Haua Chilumba amemshukuru Mhe. Mtenga kwa msaada huo na ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza na kushirikiana na kikundi hicho ili kuboresha usafi wa mazingira katika Manispaa yetu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.