*MTWARA UFUNDI YAONGOZA KITAIFA KWA SHULE ZA UFUNDI
*SHANGANI KINARA SHULE ZA KATA MKOANI MTWARA
Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeibuka kidedea kimkoa katika ufaulu wa matokeo ya kidato cha nne ambapo jumla ya wanafunzi 1,871 kati ya wanafunzi 1,934 wamefaulu mtihani huo sawa na 97% ya wanafunzi wote waliofanya mtihani.
Aidha, Manispaa imeweka rekodi mpya kwa shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa kwa shule zote za Ufundi za Tanzania Bara na nafasi ya pili Kimkoa ikitanguliwa na Shule ya Sekondari ya Abbey, wakati Shule ya Sekondari ya Shangani ikishika nafasi ya kwanza kwa Shule zote za Kata zilizopo Mkoani Mtwara.
Rekodi nyingine iliyowekwa katika matokeo yaliyotangazwa Januari 23,2025 na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ni kwa Wanafunzi wa elimu maalumu waliomaliza Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi kwa mara ya kwanza wamefaulu wote kwa kupata ufaulu wa Daraja la (2-4).
Vilevile Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeingiza Shule Sita kwenye Shule kumi Bora zilizofanya vizuri Kimkoa katika Mtihani huo
Katika Matokeo hayo jumla ya wanafunzi 317 wamepata ufaulu wa Daraja la kwanza, huku wanafunzi 328 wamefaulu kwa Daraja la pili, wanafunzi 408 wamepata ufaulu wa Daraja la tatu wakati wanafunzi 818 wamepata ufaulu wa Daraja la nne na wanafunzi 61 wamepata Daraja sifuri.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.