Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani imeweka mikakati kabambe kubaini changamoto na kuzitatua kwa Pamoja ili kukamilisha ujenzi wa majengo yote katika Hospitali ya Wilaya Mjimwema, ili ikamilike na kuanza kutoa huduma kwa wananchi hivi karibuni.
Akitoa majumuisho ya kikao kilichofanyika katika viunga vya Hoapitali hiyo kwa lengo la kuweka mikakati ya ukamilishaji wa ujenzi, Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Willy Ndabila amesema amewaagaiza mafundi kujipima kabla ya kuchukua kazi zaidi ya moja ili waendane na mikataba yao.
Amesema wamekubaliana na mafundi kuhakikisha wanakamilisha kazi ndani ya siku 14 kuanzia leo (21/03/2025) hivyo watatakiwa kukabidhi kazi ifikapo tarehe 05/04/2025.
Aliongeza kuwa, kwa upande wa Halmashauri imejipanga kufanya malipo yote kwa wakati, na kuwapatia mafundi ushirikiano mkubwa ili kufikia malengo tarajiwa.
Kikao hiko kilihusisha wataalamu toka Manispaa ya Mtwara – Mikindani wakiwemo kitengo ya Ununuzi na Ugavi, Wahandisi, Katibu wa kamati ya Ujenzi wa Hospitali, mafundi wadogo (local fundi) na wengineo.
Katika hatua nyingine, Timu ya usimamizi na uendeshaji wa huduma za afya ngazi ya Halmashauri (CHMT) imefanya usafi wa mazingira katika Hospatali hiyo ikiwa ni sehemu ya maandlizi ya kuanza kutoa huduma kitengo cha wagonjwa wa njee (OPD) pmoja na maabara.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.