Ikiwa inatarajia kuupokea Mwenge wa Uhuru Mei 25, 2025, Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeanza mikakati ya kuupokea ikiwemo kutembelea Miradi iliyopendekezwa kupitiwa na Mwenge huo.
Leo tarehe 03/04/2025, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa ndani Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Alphonce Mulima amefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi iliyopendekezwa ikiwemo, Mradi wa Ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) - Mtawanya, Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Msikitini - Kata ya Majengo, Shule ya Sekondari ya Tandika pamoja na Mradi wa Kioski Bayana cha maji (Kilula) katika Mtaa wa Mwera Kata ya Chikongola.
Katika ziara hiyo Mulima amesisitiza mafundi na wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha wanazingatia ubora wa majengo na utunzaji wa nyaraka muhimu.
Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 ni: “ Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa Amani na Utulivu”.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.