Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeshika nafasi ya kwanza kwenye usimamizi na utekelezaji wa afua za lishe kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 kati ya halmashauri tisa za Mkoa wa Mtwara.
Ushindi huo umepatikana mara baada ya Manispaa kutekeleza viashiria tisa vilivyopo kwenye mkataba wa afua za lishe vikiwemo utoaji wa fedha shilingi elfu moja kw akila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano ya fedha ambayo inatumika kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaogundulika na utapiamlo, usimamizi shirikishi kwenye vituo vya afya, maduka yanayouza cyakula na hoteli , utaoji wa matone ya viatamin A kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Viashiria vingine ni apamoja na matibabu ya utapiamlo kwa watpoto waliogundulika na ugonjwa huo, ukaaji wa vikao vya kamati ya lishe vinavyokaliwa kila robo pamoja na utoaji wa vidonge vya kuongeza wekundu wa damu kwa wamama wajawazito
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.