Kutokana na Utendaji Kazi bora wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika kushughulikia masuala yahusuyo watumishi ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Serikali Kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imeikabidhi Manispaa tuzo ya Ushindi ya Usimamizi bora wa Rasilimaliwatu baada ya kushika nafasi ya pili kati ya Manispaa ishirini zilizopo Tanzania bara katika mwaka wa fedha wa 2024/2025
Tuzo hizo zimetolewa Leo Desemba 19,2024 na Naibu Waziri wa Wizara ya Utumishi na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu Kwenye Kikao kilichowahusisha Wakuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kilichofanyika katika Ukumbi Wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Aidha tuzo hizo zimetolewa baada ya Serikali kufanya tathmini ya Utendaji Kazi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika sekta mbalimbali.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.