Manispaa ya Mtwara-Mikindani leo Novemba 27,2021 tumepokea mabati 1060 na kofia kumi na sita kutoka kiwanda cha MM Intergrated Steel Mills Ltd kw aajili ya kumalizia kazi ya kupaua madarsa ishirini na mbili ya Sekondari yanayoendelea kujengwa kupitia fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taif ana Mapmabno dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO-19 zilizotolewa na Mhe. Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Tayari mabati hayo yameshakabidhiwa kwenye shule husika na na kazi ya upauaji wa madarsa imeshaanza
Manispaa ya Mtwara-Mikindani tunafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kazi hii inakamilika kwa wakati desemba 15 mwaka huu ili wannafunzi wetu waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwakani wote waingie darasani.
Shule zilizopata fedha hizo ni Pamoja na na Shule ya Sekondari ya Chuno Tsh. 80,000,000 (Ujenzi w amadarsa manne), Shule ya Sekondari Bandari Tsh. 80,000,000 (madarasa manne), Shule ya Sekondari Shangani Tsh. 80,000,000 (Madarasa manne) na Shule ya Sekondari Mtwara-Ufundi Tsh. 40,000,000 (madarasa mawili).
Shule zingine ni Pamoja na Shule ya Sekondari Mangamba Tsh. 40,000,000 (Madarsa Mawili), Mitengo Tsh. 40,000,000 (Madarasa Mawili), Shule ya Sekondari Sino Tanzania Friendship Tsh. 40,000,000 (Madarasa Mawili) Pamoja na Shule ya sekondari ya Naliendele Tsh. 40,000,000 (Madarasa Mawili).
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.