Baada ya Manispaa ya Mtwara Mikindani kuingiziwa fedha Shilingi Milioni Mia tano sitini (560,000,000) kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kata ya Tandika, Agosti 3,2024 Mhe. Mwanahamisi Munkunda, Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Sixmund Lungu na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mwalimu Hassan Nyange wamewaongoza wananchi wa Kata ya Tandika, Viongozi wa Chama na Serikali na watumishi kushiriki kujitolea kuchimba msingi wa ujenzi wa shule hiyo mpya.
Akizungumza mara baada ya kumalizika Kwa zoezi la uchimbaji wa msingi, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara amewapongeza watumishi na wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo huku akisisitiza hkikamikikankwanujenzi wa Shule hiyo ifikapo Novemba mwaka huu ili ikifika Januari mwakani, Wanafunzi wote wa Kata ya Tandika wanaosoma nje ya kata hiyo warudi kusoma kwenye shule yao mpya.
Nae mkazi wa Kata ya Tandika Bi Fatuma Selemani Hassani amesema kuwa uwepo wa Shule hiyo katika itasaidia kupunguza gharama za nauli kwa Wazazi , kuepuka mimba zisizotarajiwa kwa Wanafunzi pia kutotembea umbali mrefu kufuata masomo.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara -Mikindani Mwalimu Hassan Nyange amesema kuwa ataendelea kuhamasisha watumishi na Wananchi kujitolea nguvu kazi ili kuokoa baadhi ya fedha ili waweze kukamilisha Miradi bila kusuasua.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.