Hadi Kufukia Septemba 2,2022 Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeshatoa chanjo ya polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano 11312 kati watoto 18770 waliolengwa sawa na asilimia 60 kwenye Kampeni ya Kitaifa ya Utoaji wa Chanjo hiyo awamu ya tatu iliyoanza Septemba 1,2022.
Takwimu hizo zimetolewa Septemba 3,2022 na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani COL. Emanuel Mwaigobeko alipotembelea vituo mbalimbali vinavyotoa huduma ya chanjo ya polio kwa lengo la kukagua na kuona zoezi hilo linavyoendelea.
Mwaigobeko amesema kuwa zoezi la utoaji wa chajo linaenda vizuri na ana imani kuw ahadi kufikia Septemba 4 Manispaa au kuvuka lengo au la utoaji wa chanjo hiyo.
Aidha ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawapelekea watoto wakapate chanjo ili kuwakinga na ugonjwa hatari wa polio.
Kmapeni ya Kitaifa ya chanjo ya polio awamu ya tatu imeanza Septemba 1,2022na itamalizika Septemba 4,2022
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.