Afisa Tarafa ya Mtwara Mjini Bwana Saidi Kayangu, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Shadida Ndile Pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya huduma za Jamii Zuhura Mikidadi wamejumuika Pamoja na wazazi na walezi wa Kata ya Mtawanya kwenye kuhuisha siku ya afya na lishe ngazi ya Kata iliyofanyika kwenye Ofisi ya Kata ya Mtawanya Leo Machi 24, 2022.
Katika zoezi hilo wazazi na walezi wamepata elimu ya namna ya kuandaa uji wa Watoto wenye virutubisho sahihi Pamoja na kupata elimu ya lishe kwa ujumla
Manispaa ya Mtwara-Mikindani imehuisha siku ya afya na lishe ngazi ya Kata kwa lengo la kuwafikia walengwa wengi kwa huduma muhimu za kuboresha afya na lishe, kuongeza kiwango cha uelewa kuhusu masuala muhimu ya afya na lishe kwa jamii Pamoja na kujadili na kuweka mkazo kuhusu majukumu ya jamii katika kutambua huduma ambazo ni stahiki zinazopaswa kutolewa na mfumo wa afya na wajibu wao katika kutumia huduma hizo
Siku ya afya na lishe itakuwa inafanyika kila baada ya miezi mitatu kwenye kila Kata ambapo shughuli za upimaji wa Watoto zitakuwa zinafanyika kwa kushirikiana na watoa huduma ngazi ya jamii (WAJA) kwa kushirikiana na wataalamu wa afya kutoka Manispaa ya Mtwara-Mikindani
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.