Ikiwa zimebaki siku tano ili kuanza kwa zoezi la Uandikishaji wa orodha ya wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapa nchini, Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange amewataka Waandikishaji wa zoezi hilo Kufanya Kazi kwa kujituma ili kuweka rekodi ya kuwa Halmashauri ya Kwanza Mkoani Mtwara Kwa Kuandikisha Wananchi wengi zaidi
Amesema kuwa ili adhma hiyo iweze kutimia Waandikishaji wanatakiwa kujitoa na kuhakikisha Kila mwananchi anaefika Kituoni anaandikishwa hata kama muda wa Kuandikishwa utakuwa umeisha.
"Tusikubali kuona hadi Siku ya mwisho kuna mtu hajaandikishwa, ninatamani kuona Wananchi wote wawe wameandikishwa ndani ya Siku nane na Siku mbili zilizobaki ziwe za kumalizia tu" amesema Mwalimu Nyange.
Aidha amewasisitiza kuzingatia lugha nzuri, yenye mvuto na busara kwa Wananchi wanaoenda Kuandikishwa huku akiwasisitiza kufanya kazi kwa kushirikiana baina yao na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata ili kazi zisikwame
Mwalimu Nyange ameyasema hayo Leo Oktoba 7,20204 Kwenye mafunzo ya Waandikishaji 118 wa orodha ya wapiga Kura iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Mtwara-Ufundi.
Zoezi la Uandikishaji linatarajia Kuanza Oktoba 11,2024 na litakamilika Oktoba 20,2024 katika vituo 111 vilivyopo kwenye Mitaa
@ortamisemi @safarimedia_ @jamiifmradio @mwalimunyange @mwaipayaabdallah @hfm94.9tz @rospamedia @kusiniyetu_online_tv @mtwaraonlinetv @faidaonlinetv
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.