MTWARA-MIKINDANI YAJIPANGA KUKUSANYA BILIONI 2.6 MSIMU WA KOROSHO 2024/2025.
Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imepanga kukusanya Shilingi bilioni mbili na milioni mia tano tisini (1,590,000,000) kwenye msimu wa korosho wa mwaka 2024/2025 ambao utahusisha chanzo cha huduma za Mji (Service Levy ) Shilingi bilioni moja na milioni mia tano (1,500,000,000).
Ushuru mwingine ni wa maegesho ya malori shilingi milioni mia mbili hamsini (250,000,000), Ushuru wa mazao Shilingi milioni tisini (90,000,000), Leseni za biashara Shilingi milioni mia mbili hamsini (250,000,000), ushuru wa malori yanayoingia mjini Shilingi milioni mia saba hamsini (750,000,000) pamoja na mfuko wa elimu
Ili Manispaa iweze kufikia lengo katika makusanyo ya zao la korosho, Leo Oktoba 18, 2024 Timu ya ufuatiliaji wa mapato yatokanayo na zao hilo Manispaa ya Mtwara-Mikindani imekutana na wadau wanaohusika na mnyororo wa zao la korosho ili kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya zao hilo.
Wadau walioshiriki kikao ni pamoja na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mawakala wa Usafirishaji wa korosho , Mawakala wa usafirishaji wa mizigo na meli pamoja na Chama Kikuu Cha Ushirika cha Mtwara na Masasi (MAMCU) ambao wamekubaliana kufanya kazi kwa timu ili malengo ya Serikali yaweze kutimia.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.