Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col.Emanuel Mwaigobeko akikabidhi jezi kwa kocha wa Timu ya Mtwara Soccer Academy Masudi Mnimbo ,zoezi hilo limefanyika April 17,2019 katika Viwanja vya Manispa
‘’Wakati watanzania wana hamu sana ya kushinda na kuona Timu ya Taifa inarudi na vikombe kama tulivyofanya juzi wakati tumewafunga timu ya Taifa ya Uganda, Manispaa ya Mtwara-Mikindani tumedhamiria kuimarisha timu za mpira za watoto’’
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Kanali Emanuel Mwaigobeko April 17, 2019 alipofanya zoezi la ugawaji wa vifaa vya michezo kwa timu ya Watoto wenye umri chini ya miaka 17(Mttwara Soccer Academy) wanaocheza mpira wa miguu.
Mwaigobeko amesema kuwa Manispaa imechukua hatua ya kuiwezesha timu vifaa vya michezo ikiwemo jezi, mipira na koni ili kuimarisha sekta ya michezo ikiamini kuwa kuwandaa vijana wadogo katika michezo itasaidia kutengeneza wachezaji bora kwenye timu ya Taifa.
“Wenzetu wanaoshinda mara nyingi huwa wanafanya maandalizi na wana vituo vidogo vinavyoendeleza michezo hivyo sisi Manispaa tutaendelea kuviwezesha vituo vidogo vya michezo vilivyopo kadiri fedha zitakapopatikana “alisema mwaigobeko
Kwa upande wake kocha wa timu hiyo Masudi Mnimbo amemshukuru Mkurugenzi wa Manispaa kwa kuwapatia vifaa vya michezo vitakavyosaidia kuendeleza vipaji vya Watoto hao.
Amesema kuwa Timu za Tanzania zinakosa washambuliaji wazuri wanaotoka nje ya nchi hivyo yeye pamoja na Timu yake watajitahidi ili Mkoa wa Mtwara uendelee kisoka.
Manispaa ya Mtwara-Mikindani inatimu 10 za Watoto wanaocheza mpira wa miguu walio na umri chini ya miaka 17,kati ya hizo tano zimeshasajiliwa na zilizobaki zinaendelea na taratibu ili ziweze kusajiliwa
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.