Kufuatia agizo lililotolewa na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamedi Mchengerwa Septemba 29,2024 lililotaka kila halmashauri hapa nchini kufanya ununuzi wa vipaza sauti kwa ajili ya Utoaji wa elimu ya mikopo na shughuli nyingine za utoaji wa elimu, Leo Septemba 10,2024, Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange amekabidhi vifaa hivyo seti 18 kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii waliopo kwenye Kata ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo hilo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano,Mwalimu Nyange amesema kuwa anayo furaha kuona ametekeleza agizo la Mhe.Waziri kwa wakati na amemshukuru kwa agizo hilo kwani vifaa hivyo havitatumika kutoa elimu ya mikopo tu bali vitatumika katika shughuli nyingine za maendeleo ikiwemo mikutano na matangazo.
“Katika kikao na Waziri, alitoa siku kumi na nne za kuhakikisha halmashari za Majiji na Manispaa zihakikishe zimenunua vifaa hivyo, Ninayo furaha sisi Manispaa ya Mtwara-Mikindani tumekeleza agizo hilo tukiwa ndani ya muda kwani leo ni siku ya kumi na tatu tangu agizo hilo lilitolewea Septemba 29,2024” amesema Mwalimu Nyange.
Aidha amewataka wataalamu waliokabidhiwa Vifaa hivyo wakiwemo Maafisa Maendeleo ya Jamii na watendaji wa Kata kuhakikisha wanavitunza na kuvisimamia ili malengo yaliyokusudiwa na Mhe. Waziri yaweze kufikiwa ikiwemo uelimishaji jamii na utoaji wa hamasa kueleka Uchagzi wa Serikali za Mitaa.
Awali akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Juliana Manyama ameishukuru Serikali kwa kuwaletea vifaa hivyo kwani itasaidia kupunguza gharama za kukodi vipaza sauti na vitarahisisha utendaji wa kazi katika kuelimisha jamii na kuifikia jamii kwa ukubwa na kwa ukaribu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.