Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Mhe. Sixmund Lungu, amekabidhi vitunzia taka (dustbin) katika Soko la Chuno (8) na Shule ya Sekondari Shangani (10) kama sehemu ya mchango wa dustbin za kisasa kutoka Ujerumani, mji wa Pforzheim.
Akikabidhi vitunzia vya taka hivyo, Mhe. Lungu aliwataka wanufaika kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuendeleza hali ya usafi katika manispaa yetu.
Alieleza kuwa jumla ya dustbin 40 zimetolewa na mji wa Pforzheim kwa ajili ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani, ambapo mbali na maeneo yaliyogawiwa, zingine zitapelekwa katika ofisi za kata, mitaa, na manispaa.
Mhe. Lungu alifafanua kwamba msaada huu unakuja baada ya Mstahiki Meya wa Manispaa, Mhe. Shadida Ndile, kufanya ziara nchini Ujerumani, ambapo aliahidiwa kusaidiwa katika juhudi za kuweka mazingira safi kwa kuletwa vitunzia vya taka hivi.
Pia alihamasisha jamii kushiriki kwenye Mbio za Mwenge zitakazofanyika siku ya Jumapili (25/5/2025)
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.