Baraza la Madiwani la Manispaa ya Mtwara-Mikindani lililoketi Januari 29,2021 katika ukumbi wa chuo cha Ualimu Kawaida limepitishwa rasimu ya Mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 yenye jumla ya shilingi 27, 745,580,924.38.
Awali akiwasilisha rasmi hiyo Kaimu MKurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Grayson Orcado amesema kuwa katika rasimu ya bajeti iliyopitishwa Manispaa imekadiria kukusanya shilingi 4,950,000,000 kutoka katika mapato ya ndani ambayo imeongezeka kutoka shilingi 4,930,000,000 iliyopangwa kukusanywa katika bajeti inayotekelezwa sasa.
Pamoja na chanzo hiko pia Manispaa inakadiria kukusanya shilingi 787,816,000 kutoka Serikali kuu kama ruzuku ya matumizi ya kawaida , shilingi 16,980,752,000 ruuzku ya mishahara na 5,027,012,924.38 ruzuku ya Miradi ya Maendeleo.
Kwa upande wa matumizi Orcado amesema kuwa Manispaa inatarajia kutumia shilingi 27,745,580,924.38 kutekeleza Miradi ya Maendeleo, kulipa mishahara na Matumizi ya Kawaida.
Aidha katika bajeti hiyo Manispaa inatarajia kutumia shilingi 2,144,451,750 kutoka katika mapato ya ndani kutekeleza Miradi ya Maendeleo.
Maandalizi ya bajeti ya mwaka ujao imezingatia vigezo mbalimbali vikiwemo Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala ya mwaka 2020/2025, vipaumbele vya wananchi vinavyotokana na jitihada za jamii, sheria ya bajeti No. 11 ya mwaka 2015, ahadi za viongozi mbalimbali wa Serikali, Mpango Mkakati wa halmshauri wa mwaka 2018/19-2022/23, wasifu wa halmashauri wa mwaka 2017 pomoja na vigezo vingine vilivyowekwa na Serikali.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.