Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeng’ara katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne na cha pili yaliyotangazwa hivi karibuni baada ya kushika nafasi ya kumi katika halmashauri zilizofanya vizuri Zaidi kati ya halmashauri 188 zilizopo hapa nchini katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne.
Aidha Manispaa pia imeshika nafasi ya tisa katika halmashauri kumi zilizofanya vizuri Zaidi katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Pili.
Katika Mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana Manispaa ilikuwa na wanafunzi waliofanya Mtihani wapatao 1659 kati ya hao wanafunzi 173 wamepata daraja la kwanza , wanafunzi 365 wamepata daraja la pili, wanafunzi 313 wamepata daraja la tatu, wanafunzi 704 wamepata daraja la nne na wanafnzi 45 wamepata daraja sifuri.
Kwa upande wa Mtihani wa Taifa wa kidato cha pili wanafunzi waliofanya Mtihani walikuwa 2191 Kati ya hao wanafunzi 377 wamepata daraja la kwanza , wanafunzi 245 wamepata daraja la pili, wanafunzi 443 wamepata daraja la tatu na wanafunzi 1042 wamepata
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.