Katika kuhakikisha kuwa Wananchi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani wanazingatia taratibu za ujenzi mjini, Manispaa ya Mtwara-Mikindani imenunua pikipiki mbili zenye thamani ya Shilingi milioni tano laki mbili (5,200,000) kutoka kwenye mapato yake ya ndani na kuzikabidhi katika Idara ya Mipangomiji na ardhi ili kusimamia na kudhibiti ukuaji wa mji kiholela.
Mkuu wa Kitengo cha Mipangomiji, Rugembe Maiga amemshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange kwa kuridhia kutoa fedha za kununua pikipiki hizo ambazo zitawezesha wataalamu kufanya ukaguzi wa kila mara na doria za kila siku ili kuhakikisha ujenzi unaofanyika ndani ya Manispaa unakidhi vigezo vya kitaalamu na vya kisheria vikiwemo Mjenzi kuwa na nyaraka za umiliki wa kiwanja na kibali cha ujenzi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2025 Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani. All rights reserved.