Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassani B. Nyange amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025 halmashauri imepanga kutumia shilingi milioni mia moja ishirini na moja (121,000,000) kutoka kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya kumaliza kulipa madeni mbalimbali ya walimu wa Shule za Msingi ambayo yatafanyika pindi mfumo wa malipo utakapofunguliwa.
Amesema kuwa katika kuhakikisha malipo hayo yanafanyika halmashuari imeshafanya uhakiki wa madeni hayo ambapo walimu 146 wa Idara ya Elimu Msingi wanadai shilingi milioni mia moja ishirini laki tisa tisini na tisa na mia tano (120,999,500).
Mwalimu Nyange ameyasema hayo leo Julai 31,2024 katika kikao cha Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Mwanahamisi Munkunda na wadau wa Elimu Wilayani hapo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yahusuyo elimu kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kawaida Mtwara (TTC).
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.