Serikali kupitia Wizara ya Afya ikishirikiana na Shirika la Nutrition International wamekabidhi Mashine ya kuchanganya madini joto kwenye Chumvi itakayotumiwa na wakulima wa Chumvi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi mashine hiyo Januari 30,2025 Afisa Lishe kutoka Wizara ya Afya ndugu Sylvester Kato amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanatumia chumvi yenye madini joto ili kujikinga na magonjwa yanayotokana na ukosefu wa madini hayo.
Amesema kuwa mashine hiyo ikitumika vema na wakulima wa chumvi katika kuchanganya madini joto itasaidia jamii kuepukana na madhara mbalimbali ikiwemo Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati (njiti), ulemavu wa viungo na uvimbe wa shingo (goita)
Aidha Ndugu Kato amemsisitiza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Ndugu Gwakisa Mwasyeba kuhakikisha Chumvi inayozalishwa na wakulima inakuwa na madini joto.
Sambamba na hilo amemtaka Mkurugenzi kutenga bajeti ya matengenezo ya mshine hiyo na kuzingatia utunzaji ili iweze kutumika kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Gwakisa Mwasyeba ameishukuru Serikali kwa kutoa mashine hiyo itayosaidia afya za wananchi wa Mtwara kuimarika na kuahidi kuisimamia vema katika kuhakikisha inafanya kazi na kuleta matokeo chanya.
Manispaa ya Mtwara-Mikindani ni mojawapo kati ya Halmashauri tano nchini zilizokabidhiwa mashine hizo zikiwemo Pangani,Mkinga,Hanang na Meatu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.