Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya amepokea msaada wa chakula Pamoja ma vifaa mbalimbali toka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kwa ajil ya kusaidia waathirika wa maafa ya mvua kubwa zilizonyesha kwa wingi wilayani hapa mapema mwenzi Februari, 2025.
Masaada huo uliokabidhiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mratibu wa maafa toka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Bi. Consolata Mbanga ni Pamoja na mahindi tani 11.028 sawa na magunia 125, Magodoro 213 Blanketi 213.
Vingine ni vyandalua 213, Sahani 213, Ndoo za lita 20 (195), mikeka Baro 50 (195), sabuni vipande 1513 pamoja na fedha kiasi cha Tsh. 13,232,000/= zilizowekwa kwenye akaunti ya Benki ya Manispaa Mtwara Mikindani kwa ajili ya kununulia maharage kilo 3308.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.