Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, leo, 14 Marchi, 2025 imesaini Mikataba 11 na mafundi wadogo (local fundi) Pamoja na wasambazaji wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo saba katika hospitali ya Wilaya Mjimwema.
Akizungumza katika zoezi hilo la utiaji Saini liliofayika katika ukumbi wa Manispaa hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Bw. Mipawa Majebele aliwataka mafundi hao kuwa na mpango kazi ,kuzingatia ubora katika ujenzi na kuthamini muda uliopangwa ili kufikia malengo tarajiwa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Manispaa Mtwara Mikindani, Willy Ndabila alisema utiaji Saini huo unakuja baada ya manispaa kupokea jumla ya shilingi 1.5 bilioni kutoka Serikali kuu kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa Hospitali hiyo inatarajiwa kuwa msaada mkubwa wa wananchi na Mtwara na maeneo Jirani.
Alisema jumla ya majengo saba yanatarajiwa kujengwa ikiwemo wodi ya Watoto (pediatric), jengo la kuhifadhia maiti (mortuary block), wodi ya kisasa (Grade one ward), jengo la kufulia (laundry Block), jengo la upasuaji(Theatre block), wod ya wanaume (medical ward male), Pamoja na wodi ya wanawake(medical ward female).
Kwa upande wao wasambazaji wa vifaa waliomba Manispaa kulifanyia kazi suala la changamoto za miundombinu kama lipo ili kufurahisha ufikaji wa maeneo husika kwa wakati.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.