Mkurugenzi wa Maniispaa Mtwara-Mikindani bi beatrice Dominic pamoja na Mstahiki meya Geofery Mwanichisye wakisaini mkataba wa usimamizi wa miradi ya TSCP na kampuni ya LEA Associates South Asia Ltd hawapo kwenye
Manispaa ya Mtwara-Mikindani imesaini mkataba wa dola za kimarekani 737,450 na mhandisi mshauri kutoka Kampuni ya Lea Associates South Asia Ltd ya India kwa ajili ya usimamizi wa miradi ya uendelezaji Miji na Majiji Mkakati (TSCP) inayotarajiwa kuanza mwezi Juni mwaka huu.
Miradi itakayokayosimamiwa ni pamoja na Ujenzi wa barabara ya Chuno,Shangani,Senegal na COTC kwa kiwango cha Lami, Ujenzi wa stendi ya Mikindani, UJenzi wa sehemu za kupumzikia ikiwemo mashujaa, Tilla, na maduka makubwa, Ujenzi wa soko chuno pamoja na ujenzi wa mfereji mkuu wa kuondoa maji kutoka skoya, Nabwada hadi baharini
Aidha utekelezaji wa miradi yote hiyo utaghrimu kiasi cha shilingi bilioni 21.7 fedha ambazo zinatolewa na benki ya dunia kama mkopo kwa Serikali na utekelezaji wake utaanza mwezi Juni mwaka huu.
Mradi wa uendelezaji miji mkakati ulianza kutekelzwa rasmi Manispaa Mtwara-Mikindani mwaka 2010 na umejenga babara nne kwa kiwango cha lami, Dampo la kisasa lililopo Mangamba pamja na vizimba 25 vya kuhifadhia takangumu, Ukarabati wa Ofisi mbalimbali za halmashauri, Ununuzi wa mitambo ya kuzolea takangumu, Ununuzi wa magari sita ya Ofisi pamoja na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya Ofisi ikiwemo Kompyuta na kuwajengea uwezo watumishi mbalimbali wa manispaa.
Mkataba uliosainiwa April 18,2018 utadumu kwa miezi 28 hadi kukamilika kwake na na mwezi Mei mwaka huu mtaalamu mshauri ataanza kazi rasmi
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.