Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeshika nafasi ya kwanza Kimkoa kwenye Matokeo ya Kitaifa ya Mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi (PSLE 2022) kwa kupata ufaulu wa asilimi 91.12 kati ya Halmashauri 9 zilizopo Mkoani Mtwara.
Katika Mtihani huo wanafunzi 2856 wakiwemo KE 1466 na ME 1390 walifanya Mtihani na waliofaulu ni wanafunzi 2576 wakiwemo Ke 1332 na ME 1244 sawa na asilimia 91.2.
Shule zilizofanya vizuri kwa matokeo ya jumla (zilizopo kwneye kumi bora) katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani ni Pamoja na Shule ya King David, Mtwara Heritage, Medi, Salem , Maendeleo, Kambarage, Shangani, Rahaleo, Mangamba na Ligula huku Shule ya Singino ikishika nafasi ya mwisho ikifuatiwa na shule ya Msingi Lwelu na Mkangala.
Kwa upande wa shule za Msingi za Serikali zilizotokea kwenye kumi bora ni pamoja na shule ya Msingi ya Maendeleo, Kambarage, Shangani, Rahaleo, Mangamba, Ligula, Mjimwema, Misufini na Likonde
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.