*Ufaulu Waongezeka Kwa asilimia 7
*Shule za Sekondari Zachuana na Binafsi
Katika matokeo ya Mtihani wa taifa wa darasa la saba yaliyotangazwa Oktoba 30,2021 na Katibu Mtendaji wa baraza la Mitihani Tanzania Dkt. Charles Msonde Manispaa ya Mtwara-Mikindani tumeshika nafasi ya pili kimkoa kati ya halmashauri tisa zilizopo Mkoani Mtwara kwa kufaulisha wanafunzi 2443 kati ya wanafunzi 2667 Waliofanya Mtihani sawa na asilimia tisini na mbili.
Ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia saba kutoka ufaulu wa asilimia 85 kwa matokeo ya Mtihani huo mwaka uliopita na kushika nafasi ya tatu kimkoa.
Matokeo hayo pia yamekuwa mazuri kwa shule zetu za Serikali za Shangani, Kambarage, Mjimwema na Namayanga ambazo zimefaulisha kwa asilimia 100 sawa na Shule za binafsi za Medi, Heritage , King David, na Salem ambazo na zenyewe pia zimefaulisha kwa wastani huo huo.
Shule zote zilizobaki zimefaulisha kwa wastani wa kuanzia asilimia 98 hadi asilimia 71 isipokuwa kwa Shule ya Msingi ya Lwelu ambayo imefaulisha kwa asilimia 58.90.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani anawapongeza walimu ,wazazi kwa Matokeo haya mazuri ambayo yameleta furaha kwetu kuwataka kuendleza mshikamano ili mwakani matokeo yawe mazuri Zaidi. Aidha amewapongeza Idara ya Elimu Msingi kwa kusimamia vizuri na ufuatiliaji ulio makini.
Hakika Mtwara-Mikindani mwaka huu tulikuwa tuna jambo letu kama kauli mbiu ya wahitimu ilivyokuwa inasema na mwakani tunakwenda na Kauli mbiu ya Ufaulu wa asilimia mia moja .
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.