Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imetekeleza jumla ya Miradi mitano ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi milioni 962/- Fedha zilizotolewa na serikali kuu na jumla ya shilingi milioni 710/- mapato ya ndani kwa mwaka 2021/2022.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu, Gwakisa Mwasyeba, akimuwakilisha Mkurugenzi wa Halmashairi hiyo, Mwalimu Hassan Nyange, wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika jana 21/11/2024 katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara Ufundi maarufu kama Masandube.
Akisoma Taarifa ya Utekelezaji, Mwasyeba aliitaja Miradi hiyo kuwa ni pamoja na Ujenzi wa Jengo la wazazi, Upasuaji, kufulia na barabara za watembea kwa miguu kituo cha afya Ufukoni.
Mradi mwingine ni Ujenzi wa Ofisi ya Ardhi na Mipangomiji pamoja na Ujenzi wa Mabweni mawili (2) shule ya Sekondari ya Wasischana Mtwara.
Mingine ni Ujenzi wa bweni moja Shule ya sekondari Mtwara Ufundi na Ujenzi wa shule ya sekondari Likombe (Madarasa 8, Maabara 3, Jengo la utawala, Maktaba, Jengo la TEHAMA, Matundu ya Vyoo 20 wavulana na wasichana, Tank la maji Ardhini, Mnara wa Tanki).
Kikao hicho kilichofunguliwa na Mkuu wa Wilaya Mtwara, Mhe. Abdalah Mwaipaya ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao, kilipokea pia Taarifa za utekelezaji miradi toka Halmashauri zingine za Nanyamba na Wilaya ya Mtwaram, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa dini na Viongozi wa vyama vya siasa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.