Mkugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassani Nyange Amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka wa Fedha 2024/2025 serikali imetenga Bajeti ya Shilingi Milioni Mia tano sitini (560,000,000,) kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari Kata ya Tandika itakayowaondolea kero wanafunzi ya kutembea umbali mrefu kupata elimu.
Akizungumza katika Mkutano wa kukusanya kero za wananchi wa Kata ya Tandika uliofanyika Machi 15,2024 Mwalimu Nyange amewaomba wazazi na walezi wa kata hiyo kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano na kuunga Mkono jitihada za serikali kwa kuchangia kujitolea nguvu kazi pindi mradi wa ujenzi wa shule hiyo utakapoanza ili fedha zitakazobaki ziweze kutatua changamoto ya shule nyingine chakavu zilizopo ndani ya kata hiyo.
Amesema kuwa wazazi watumia fedha nyingi katika kuwasomesha Watoto kike hivyo atawachukulia hatua kali za kisheria wanaume (wahuni) wanaorudisha nyuma au kuzizima ndoto za wanafunzi kwa kuwapatia mimba huku akisisitiza jamii kuendelea kuwalinda Watoto dhidi ya ukatili mbalimbali ukiwemo ubakaji na ulawiti.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi amewapongeza wananchi wa kata hiyo kwa kuonesha jitihada katika kila mtaa kujenga ofisi za serikali za mitaa.
Akitolea ufafanuzi suala la mikopo ya wanawake vijana na watu wenye ulemavu Mkurugenzi alisema kuwa hivi karibuni serikali itatoa maelekezo kwa fedha hizo kwani zinaendelea kutengwa.
Diwani wa Kata ya Tandika Mhe Haroun amesema kuwa ofisi yake iko wazi Kwenda kutoa kero pongezi pamoja na kushirikishana mambo mazuri ya maendeleo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.