Kutokana na uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa Surua na Rubella wataalamu wa faya kupitia kitengo cha afya kinga Manispaa ya Mtwara-Mikindani wameendelea kutoa huduma ya chanjo ya Surua na Rubella kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano amabo hawajapata au kukamilisha chanjo hiyo.
Zoezi la utoaji wa chanjo ya Surua na Rubelaa limeanza februari 20 na linatarajia kumalizika Februari 27 mwaka huu, ambapo wahudumu wa afaya wanapita nyumba kwa nyumba ili kuwabaini watoto ambao hawajapata chanjo na kuwapatia chanjo hiyo.
Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani inatoa chanjo ya Surua na Rubella mara baada ya kubainika kwa uwepo wa vimelea vya ugonjwa jhuo kutoka kwa wagonjwa kumi na nne wakiwemo wagonjwa sita wa Surua na wagonjwa nane wa Rubella.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.