Katika kuhakikisha kuwa changamoto ya uhaba wa madawati katika shule za Msingi inatatuliwa, Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupitia mapato yake ya ndani imetumia shilingi 110,500,000 kutengeneza madawati 850 ya shule za Msingi.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi madawati hayo kwa walimu wakuu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Shadida Ndile amewataka walimu na wanafunzi kuyatunza madawati hayo ili yatumike kwa muda mrefu.
Shadida amesema kuwa Manispaa inatambua changamoto zilizopo shuleni na kuahidi kuzitatua changamoto hizo awamu kwa awamu kwa kushirikiana na Mkurugenzi Pamoja na wazazi.
AidhaShadida amewaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu vizuri katika Mitihani yao.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake Khaira Selemani mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mivinjeni amemshukuru Mkurugenzi kwa kuwapelekea madawati na kuahidi kuyatunza madawati hayo na kwamba watasoma kwa bidii ili waweze kufaulu mitihani yao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.