Manispaa ya Mtwara-Mikindani inazidi kung'ara kwa upande wa usimamizi wa matumizi mazuri ya fedha na kupelekea kupata hati safi kwa mara ya sita mfululizo kuanzia mwaka wa fedha 2015 hadi mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Katika ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha wa 2020/2021 Manispaa ya Mtwara-mikindani ilikuwa na hoja sihirini na sita (26) kati hizo hoja kumi na moja (11) zimefungwa na hoja kumi na tano (15) zipo kwenye utekelezaji.
Bwana Festick Mwampashe mwakilishi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Mkoa wa Mtwara ameipongeza Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kupata hati safi (unqualified opinion) katika mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Manispaa ya Mtwara-Mikindani tunaahidi kuendelea kuchapa kazi kwenye kusimamia matumizi ya fedha za Serikali ili tuendelee kupata hati safi muda mara zote.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.