Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imewasisitiza waombaji wa mikopo ya asilimia kumi (10%) kwa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu kuzingatia taratibu zote za msingi wakati wa kuomba mikopo hiyo ili kuepusha kukosa sifa za kupata mikopo.
Akiongea wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo vikundi vyenye nia ya kuomba mikopo hiyo, Mratibu wa mikopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Bi. Rida Kahungenge amesema ni vema vikundi husika kufuata taratibu zilizoinishwa ili kupata mikopo hiyo.
Ametajata taratibu hizo ikiwemo, usajili wa vikundi katika mfumo wa kielektroniki wa utoaji mikopo, pamoja na kuzingatia kuandaa andiko mradi.
Bi. Kahungenge alisema mafunzo hayo yanafuatia baada ya kuona vikundi vingi vinashindwa kuandaa andiko mradi na taratibu zingine muhimu.
Aidha ametoa rai kwa washiriki wa mafunzo hayo kuepukana na tabia zinazoweza kufifisha urejeshaji mikopo, ikiwemo tabia ya talaka holela na nyinginezo.
Kwa mujibu wake, vikundi zaidi ya 100 vimeshiriki mafunzo hayo yaliyofanyika leo Oktoba 18, 2024, katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu (TTC) kawaida.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.