Manispaa ya Mtwara-Mikindani Kupitia kikao cha kamati ya fedha na uongozi kimepitisha fedha kiasi cha shilingi milioni 134 Kutoka kwenye mapato yake ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 17 pamoja na ununuzi wa madawati na meza 160.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Ernest Mwongi alipokuwa anawasilisha taarifa ya miundombinu ya shule za Sekondari na mapokezi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2019, kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya kilichofanyika desemba 18,2018 katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha SAUT.Mtwara.
Amesema kuwa uamuzi huo umefanyika baada ya kuwa na changamoto ya ukosefu wa madarasa,madawati na meza kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2019.
“Mpaka sasa Manispaa tunao uwezo wa kuchukua wanafunzi wa kidato cha kwanza 1200 lakini kutokana na ufaulu kuwa mkubwa mwaka huu wanafunzi 1860 wamefaulu ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 660, ili wanafunzi wote waliochaguliwa wakae darasani tunahitaji madarasa 17 pamoja na viti na meza 660” alisema Mwongi.
Ameongeza kuwa fedha zilizotolewa hazitaweza kumaliza changamoto iliyokuwepo hivyo Manispaa imeweka mikakati ya kuwasiliana na wadau wake ili kuweza kutia nguvu katika kutatua changamoto mbalimbli za elimu.
Ujenzi wa madarasa unatarajia kuanza mapema wiki ijayo kwa kutumia mafundi wenyeji ni matarajio kuwa ujenzi huo utakamilika kw awakti ili wanafunzi hao wawezekuingia darasani ifkapo Januari 2019
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.