Ili kuweka mazingira rafiki ya wafanyabiashara wa Soko Kuu la Vigaeni, Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imetoa fedha Shilingi milioni thelathini na tisa laki tisa themanini na moja mia tano sabini na tano (39, 981,575) kutoka kwenye mapato yake ya ndani kwa ajili ya kufanya ukarabati wa soko hilo katika eneo la wafanyabiashara wa mbogamboga “Mkunguni” ambapo Manispaa imepekeka Shilingi milioni ishirini (20,000,000) fedha za awamu ya kwanza kati ya Shilingi milioni thelathini na tatu (33,000,000) zilizotengwa kwa ajili ya kuwekea zege, kuchimba mifereji ya maji ya mvua, kuweka nguzo za chuma na kupaua kwenye baadhi ya sehemu ya eneo hilo ambapo ukarabati umeshaanza.
Aidha Shilingi milioni tano laki moja (5,100,000) zimepelekwa kwa ajili ya kukarabati jengo la Nafaka kwa kuweka umeme utakaowezesha wafanyabaishara hao kufanya biashara hata nyakati za usiku na Shilingi Milioni kumi na nne laki nane themanini na moja mia tano sabini na tano (14,881,575) za ukarabati wa choo cha soko hilo kwa awamu ya pili
Bi Salma Issa Waziri Mfanyabiashara wa Mbogamboga katika soko la Mkunguni ametoa shukurani zake kwa Mkurugenzi wa Manispaa Mwalimu Hassan Nyange na watumishi wake kwa kutatua changamoto zinazowakabili na kuwasimamia vizuri wafanyabiashara hao.
“Mkurugenzi ameamua kututengenezea soko letu liwe vizuri, tulikuwa na changamoto ya kujaa kwa maji hasa katika kipindi hiki cha mvua, lakini kwa sasa zoezi hili likimalizika tutafanya biashara kwa utulivu tunashukuru na tumefurahi “amesema mfanyabiashara huyo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.