Mkuu wa Mkoa wa Mtwara BRIG. Jen Marco Gaguti Agosti 3, 2021 amezindua rasmi chanjo ya UVIKO-19 Mkoani Mtwara katika Kituo cha Afya Likombe huku akitoa maagizo kwa wamiliki kuzingatia ukaaji wa abiria kwa kutosimama abiria (abiria wote wakae kwenye viti)
“Kwa Mkoa wetu wa Mtwara kuanzia leo,vyombo vyote vya usafiri tuzingatie ukaaji wa abiria, msizidishe wala kusimamisha abiria, bila kusahau maji safi na sabuni kwaajili ya kunawa katika vituo vyenu vya abiria” Amesema Gaguti
Ili kufanikisha zoezi hili chanjo katika Mkoa wa Mtwara, Mhe Gaguti amewataka wananchi kufuata maelekezo na kutoa ushirikiano kwa wahudumu wa afya katika vituo vilivyoainishwa.
Wakati zoezi hili likiendelea, Mhe. Gaguti ameendelea kutoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo jinsi ya kujinga na maambukizi ya UVIKO19.
Zoezi la utoaji chanjo ya UVIKO-19 limezinduliwa leo na litaendelea katika vituo vyote vilivyoanishwa na Manispaa ya Mtwara-Mikindani chanjo inatolewa katika Vituo vya Afya Mikindani na Mikindani na Hospitali ya Rufaa ya Ligula.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.