Katika kuhakikisha kuwa Wilaya ya Mtwara inafanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani ya taifa ya kumaliza elimu ya Msingi na Sekondari , Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya Septemba 19,2022 katika Ukumbi wa Chuo Cha Ualimu Kawaida, amezindua miongozo ya elimu na kuikabidhi Kwa Maafisa Elimu Kata wa halmashauri tatu zilizopo Wilaya ya Mtwara huku akiwataka walimu kufundisha kwa bidii ili Wilaya iweze kushika nafasi tatu za juu Kimkoa kwenye matokeo ya mitihani ya Taifa.
“Nimekabidhi miongozi hii kwenu ninaomba mkaisimamie, Mimi kama Mkuu wa Wilaya nitafarijka kuona nafasi ya kwanza hadi ya tatu ndani ya Mkoa wetu inashikwa na Wilaya yangu kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa ya Kumaliza elimu ya Msingi na Sekondari’amesema Mhe.Kyobya.
Katika kuhakikisha kuwa malengo ya kuongeza ufaulu yanafikiwa, Mkuu wa Wilaya amewasititiza wadau wa elimu kuanzia ngazi ya chini hadi Wilaya kuweka mikakati ya ufaulu ikiwemo uwezeshaji wa upatikanaji wa chakula shuleni kwa kuanzisha bustani kwa ajili ya kulima mazao ya chakula pamoja na udhibiti wa utoro kwa wanafunzi.
“Wekeni mikakati ya watoto wale,tena wale kwelikweli ili wasipate kisingizio cha kwa nini walifeli, mkatengeneze bustani kwa ajili ya ulimaji wa mazao ya chakula na kama eneo la shule ni kubwa basi mkalime na ya biashara ili iwe sehemu ya kipato cha shule “.
“Lakini pia hakikisheni mnafahamu Watoto wangapi hawajafika shule, mjue wako wapi,wanafanya nini na mchukue hatua za kisheria kwa wazazi na walezi ambao Watoto wao hawaendi shule “ amesema Mhe.Kyobya
Aidha amewasisitiza Wakurugenzi kuhakikisha wanaisimamia miongozo hiyo na kuwafikia wadau wote wa elimu ambao wataijadili kwa kina na kufanyia kazi ili kuleta mabadiliko chanya kwenye elimu .
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Mtwara Thomas Salala amewasisitiza walimu kuifanyia kazi miongozo iliyotolewa kwa kujitoa kufanya kazi kwa bidi ili kuwajenga wanafunzi wetu kwenye misingi imara ya kujifunza na hatimae waweze kufanya vizuri kwenye mitihani yao.
Akizungumza kwa niaba ya Maafisa elimu wenzake bwana Afisa Elimu kutoka halmashauri ya Wilaya ya Mtwara amesema kuwa yeye pamoja na wenzake wamejiandaa vema katika kuisimamia miongozo hiyo ili iweze kuleta matokeo chanya na kwamba
Nae mwalimu hilda Lukanga ameipongeza Serikali kwa kutoa miongozo hiyo na kwamba wao wapo tayari kuisimamia lakini pia ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanatoa ushirikianokwa walimu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.