Baada ya kufanikiwa kutatua kero ya kuvuja kwa soko la Nafaka lililopo soko kuu ambapo Halmashauri ilitumia shilingi milioni hamsini (50,000,000) kutoka mapato ya ndani kwa kuezua na kuweka bati mpya mwaka uliopita, Mwalimu Hassani B. Nyange Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ameahidi kuweka sakafu na kujenga mifereji ili kutatua kero ya kutuama kwa maji wakati wa mvua katika Soko la matunda na mbogamboga(Mkunguni) katika bajeti ya mwaka 2024/2025.
Aidha Nyange ameahidi kutumia shilingi milioni ishirini (20,000,00) katika bajeti hiyo kwa ajili ya ujenzi wa matundu kumi ya vyoo ili kuepusha uchafuzi wa mazingira hususani wakati wa usiku soko hilo linapokuwa limefungwa.
Amesema hayo Agosti 5,2024 katika kikao cha Mkuu wa Wilaya na Wafanyabiashara wa Soko Kuu Mtwara-Mikindani kilicho fanyika katika Stendi kuu ya zamani ya Mabasi kwa lengo la kujadili changamoto na maoni ya wafanya biashara ili kutatua changamoto zinazowakabili.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.