Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange Leo Aprili 8,2024 amezungumza na watumishi kutoka Idara mbalimbali ili kuweka mikakati kabambe itakayokayopelekea Manispaa kuendelea kufanya vizuri kwenye Mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru tarehe 25.05.2025.
Akizungumza katika kikao hiko kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Chuo Cha Ualimu cha Mtwara Ufundi, Mwalimu Nyange amesema kuwa, anatamani katika Mbio za Mwenge wa mwaka huu Manispaa iendelee kushika nafasi ya kwanza Kimkoa kama ilivyokuwa mwaka uliopita, na kupandisha nafasi katika upande wa Kanda na Kitaifa kwa kushika nafasi za juu.
Amesema kuwa hayo yote yatawezekana endapo kila mmoja katika nafasi yake atashiriki kikamilifu kuanzia hatua za awali za maandalizi hadi siku ambayo Manispaa itapokea Mwenge huo.
Mwenge wa Uhuru mwaka huu unaenda na Kauli Mbiu inayosema “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu Wa Mwaka 2025 Kwa Amani Na Utulivu”
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.