Sekondari ya Rahaleo ametoa zawadi ya fedha shilingi milioni mbili (2,000,000) kwenye sherehe ya kuhitimu kidato cha nne kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kujipima na kwa walimu wa Taaluma wa kidato cha nne na kidato cha pili pamoja na wapishi wa Shuleni hapo.
Ismail Dadi ni miongoni mwa mwanafunzi aliepata zawadi ya fedha taslimu ya Shilingi laki tatu (300,000) na cheti kwa kuwa mwanafunzi bora katika masomo yote na
Kundi lingine lililopata zawadi ni kundi la wanafunzi kumi na moja bora waliofanya vizuri katika masomo mbalimbali ambao wamezawadiwa Shilingi laki tano na elfu hamsini (550,000),
Aidha Wanafunzi wawili walioboresha ufaulu wao wamezawadiwa Shilingi laki moja (100,000) na wanafunzi watano waliopata daraja la kwanza katika kipindi chote cha masomo shuleni hapo wamezawadiwa Shilingi (50,000) kwa kila mmoja.
Vilevile katika sherehe hiyo Mwalimu nyange ametoa zawadi ya fedha Shilingi laki sita (600,000) kwa Walimu wa taaluma 13 wa kidato cha pili na kidato cha nne waliofaulisha vizuri kwenye masomo mbalimbali kwa mwaka 2023/2024 na ametoa zawadi ya shilingi laki moja (100,000) kwa wapishi wawili shuleni hapo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.