Kuelekea zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27,2024 hapa nchini, Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia kura Manispaa ya Mtwara-Mikindani wamehimizwa kufanya Kazi hiyo Kwa kujituma na Kwa uzalendo mkubwa ili zoezi hilo litamatike Kwa amani na utulivu.
Wito huo umetolewa Leo Novemba 23,2024 na Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassani Nyange alipofungua semina ya siku moja kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia kura.
Aidha Mwalimu Nyange amewataka Wasimamizi hao kujiamini na kuwa wasikivu wakati wote wa mafunzo ili wakaifanye kazi vizuri
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.