Wakati Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania ikishirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI ikiendesha mafunzo ya siku tatu kwa walimu wa shule za Sekondari wanofundisha kidato cha kwanza kuhusu utekelezaji wa mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2023, Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani amewataka walimu hao kuwa na utayari wa kupokea maelekezo ya mtaala mpya na kuyafanyia kazi kwa vitendo ili kutimiza malengo ya Serikali.
Amesema kuwa baada ya mafunzo hayo kumalizika, Manispaa ya Mtwara-Mikindani itaunda kamati ndogo ya kupitia yale yote yaliyojadiliwa kwenye mafunzo kuhusu mtaala mpya nakuona namna ya kuyatimiza.
Mafunzo hayo ambayo yanafanyika kwa walimu wote wanaofunsiha kidato cha kwanza mkondo wa jumla na kidato cha pili mkondo wa amali kwa shule za Serikali na zisizo za Serikali Tanzania bara na Visiwani , yanalenga kukuza uelewa wa jumla kwa walimu kuhusu maboresho ya mtaala wa Elimu ya Sekondari hatua ya chini kwa mKondo wa jumla na mkondo wa amali.
Kwa Manispaa ya Mtwara-Mikindani mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tatu kuanzia Leo Januari 6,2024 na yatakamilika Januari 8,2025 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi na jumla ya walimu 212 watapatiwa mafunzo hayo
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.