Baada ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupeleka fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye Kata,Shule na Vituo vya afya Shilingi milioni 543,440,000 za mapato ya ndani na Shilingi bilioni 2,073,822,000 zilipokelewa hivi karibuni kutoka Serikali Kuu, Leo Desemba 6, 2024 Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mwalimu Hassan Nyange amekutana na wazabuni wanaofanya kazi ya kusambaza vifaa vya ujenzi na kuwataka kufanya kazi kwa weledi pale watakapopata kazi hiyo huku akiwahakikishia kuwalipa kwa wakati.
Amesema kuwa Manispaa inawategemea, inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na wafanyabaishara hao kwenye utekelezaji wa miradi na shughuli nyingine na kuwasihi kuendelea kuthamini na kulinda mji wao Mtwara kwa kufanya kazi kwa weledi na kwa uaminifu mara zote wanapopata kazi ili miradi ikamilike kwa wakati.
Kwa upande wa wafanyabiashara hao wamempongeza Mkurugenzi wa kukutana nao na kujadiliana kuhusu maendeleo ya Mji wao na kuomba vikao kama hivyo viwe vinafanyika mara kwa mara ili kujenga mahusiano mazuri.
Mbaraka Manzi mfanyabaishara wa vifaa vya ujenzi amewasihi wafanyabiashara wenzake kuimarisha mahusiano na Ofis ya Mkurugenzi , kuwa waaminifu, kuthamini kazi wanazopata na kuhakikisha wanapopata kazi ya kupeleka malighafi wafanye kwa wakati ili kutowaangusha watumishi.
Aidha baada ya kikao hiko wazabuni hao na timu ya wataalamu walitembelea mradi wa ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi inayojengwa Shangani Magharibi kwa gharama ya Shilingi milioni mia moja themanini (180,000,000) amabpo ujenzi umefikia asilimia 45 pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari Kata ya Tandika inayojengwa kwa gharama ya Shilingi milioni mia tano sitini (560,000,000) na ujenzi wake umefikia asilimia 97
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.